Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba yangu amehamia Yanga sababu ya Chama - Kamwe

Kamwe Bababa Baba yangu amehamia Yanga sababu ya Chama

Tue, 2 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema tangu wamtambulishe kiungo mshambuliaji Clatous Chama kutoka Simba Sc, wamepokea wanachama wapya wa Simba wengi sana ikiwemo na Baba yake Mzazi.

"Wengi wanauliza mpaka sasa tumenufaika vipi na utambulisho wa Chama. Mpaka sasa tumepokea taarifa za mashabiki wa upande wa pili ambao wamehamia Yanga akiwemo Baba Kamwe nae amemfuata Chama. Wote waliohama akiwemo baba yangu, tunawaandalia siku maalumu ya kuwapokea.

“Baba amehama na yeye, amekuja na Mwamba wa Lusaka, tutamtambulisha nay eye kwamba katika mashabiki 3000 wa Simba waliohama na Chama, baba yake na Ally Kamwe naye yumo. Alinifuata akaniambia kwa siri lakini mimi friji langu ni bovu nimevujisha siri na anisamehe.

"Mashabiki wa Simba zaidi ya 3000 wamehamia Yanga akiwemo na baba yangu mzee Shabani Kamwe kwa sababu ya raha za Chama ambazo wanaamini watakuja kuzipata huku, hiyo ndio moja ya faida ya kumsajili Chama kwani unapata vitu vingi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live