Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Luis Diaz afunguka yaliyomsibu alipotekwa

IMG 6267.jpeg Baba wa Luis Diaz afunguka yaliyomsibu alipotekwa

Sun, 12 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Luis Manuel Diaz, Baba mzazi wa mshambuliaji wa Liverpool Luis Diaz amezungumza kwa mara ya kwanza tangu aachiwe huru.

Akiongea kwa hisia kubwa hata kulia mzee Diaz (58) alisema " walinilazimisha nitembee sana, bila kupumzika vizuri, tukiwa milimani kwenye mazingira magumu sana".

"Nisingetaka mtu yoyote awe kule milimani na kwenye hali kama niliyokuwepo mimi"

"Ulikuwa wakati mgumu sana kwangu, sijalala vizuri siku 12".alisema mzee Diaz huku akilia kwa uchungu.

"Watekaji walinihimiza kuwa mtulivu, japo walinihudumia vizuri lakini sikuwa na raha"

Mzee Diaz na mke wake Bi.Cilenis Marulanda walitekwa mnamo Oktoba 28 katika mji wa Barrancas nchini Colombia.

Polisi walifanikiwa kumuokoa mama huyo masaa machache baadae, huku watekaji wakiendelea kumshikilia mzee Dia.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live