Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Ansu Fati amjia juu Xavi kutomchezesha mwanae

Bori Fati & Ansu Fati Baba wa Ansu Fati amjia juu Xavi kutomchezesha mwanae

Wed, 29 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bori Fati (baba yake Ansu): "Sijui kwa nini Xavi hamchezeshi Ansu. lazima awe na sababu zake. Ansu hana kinyongo naye, kwani Xavi alikuwa mchezaji aliyemkubali siku zote. lakini mimi kama baba nina hasira sana."

"Inanisumbua jinsi wanavyomchukulia Ansu. wanampa dakika 1, 2 na 3. nimesikitishwa sana, Ansu alistahili mengi zaidi."

"Ansu hataki kuondoka Barca, lakini nataka kumuona akifanikiwa, nina hasira na klabu. katika mwezi mmoja tutakutana na Jorge Mendes."

"Sitaikosoa Real Madrid kwa sababu maisha yana mambo mengi na huwezi kujua nini kinaweza kutokea."

"Mateu Alemany ananiambia kuwa Ansu ni sehemu ya urithi wa klabu, mimi kama baba nimemwambia Ansu ni bora aondoke lakini Ansu ameniambia hakubaliani na mimi katika hili anataka kubaki. ."

"Kama ingekuwa juu yangu, ningeondoka Barca kesho. Nilimwambia Ansu kwamba ikiwa hali haitabadilika, tutalazimika kuondoka

Chanzo: www.tanzaniaweb.live