Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Akram Afif awakataa Wasomali

Akram Afif Qatar Afc Asian Cup 2023 1707585370 129028 Baba wa Akram Afif awakataa Wasomali

Wed, 14 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Somalia watu walikuwa wakijuvunia sana mafanikio ya nyota wa timu ya taifa ya Qatar, Akram Afif, wakiamini ni msomalia mwenzao.

Hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi nchini humo wanadhani baba wa staa huyo, Hassan Afif, ni msomali mwenzao.

Lakini sasa baba wa staa huyo mzee Hassan Afif amevunja ukimya na kusema mwanaye siyo msomali bali ni mqatari.

Hassan Afif pia ametegua kitendawili kuhusu yeye mwenyewe akisema yeye siyo msomali bali myemeni aliyezaliwa Tanzania.Kwa kifupi Hassan Afif amewakataa jumla wasomali.

Dhana ya wasomali kwamba Hassan Afif ni msomali mwenzao inatokana na ukweli kwamba enzi za Unaona wake aliwahi kucheza soka nchini humo kwenye klabu ya Horseed.

Ni kupitia muunganiko huo ndiyo maana wasomali wanadhani Hassan Afif ni msomali mwenzao, na kama ni msomali mwenzao basi na watoto wake, akiwemo Akram, ni wasomali wenzao.

Lakini kauli ya Hassan Afif imemaliza mjadala. Mwanaye ni raia wa Qatari, Yeye ni raia was Yemen aliyezaliwa Tanzania, fulstop.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live