Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba wa Aaron Ramsdale afichua mazito

Aaron Ramsdale .png Baba wa Aaron Ramsdale afichua mazito

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba wa Mlinda Lango wa Arsenal, Aaron Ramsdale amedai mtoto wake hana furaha na amepoteza tabasamu lake kwani klabu hiyo imemtosa chini ya kocha Mikel Arteta.

Baba wa Mlango huyo zamani wa Sheffield United na Bournemouth mwenye umri wa 25, aliwasili Emirates mwaka 2021 na moja kwa moja akaingizwa kwenye kikosi cha kwanza lakini sasa ameanza kusugua benchi tangu Septemba mwaka huu.

Mlinda Lango mpya aliyesajiliwa na Arteta kwa mkopo David Raya, ndiye amechukua nafasi ya Ramsdale tangu Septemba kwenye ushindi dhidi ya Everton.

Raya ambaye ni raia wa Hispania kwa sasa amekuwa chaguo namba moja wa Arteta na mechi pekee ambayo Ramsdale alicheza ilikuwa kwenye michuano ya Kombe la Carabao dhidi ya West Ham.

Ramsdale alikiri mwezi uliopita kwamba anaumia sana na kuteseka baada ya namba yake kupokwa lakini ameapa kupigania nafasi yake Arsenal.

Baba yake mzazi, Nick Ramsdale, amezungumzia kuhusu mustakabali wa mtoto wake huyo kwenye kikosi cha Arsenal akisema: “Aaron amepoteza tabasamu lake, ni ngumu sana tukimuona akiteseka kwa sababu tunapenda aendelee na tabasamu lake.”

Nick kisha alifichua mazungumzo kati yake na Arteta na kudai kwamba kocha huyo alimweleza wazi kwamba Ramsdale ndio chaguo lake, licha ya wakala wa Raya hivi majuzi kusema kwamba kipa huyo aliwindwa kwa muda mrefu Arsenal. “Haiwezakeni kwa jinsi mambo yanavyokwenda.”

“Hatujui sababu ni nini. Ramsdale anafanya kazi kubwa sana Arsenal ishinde taji la ligi.”

Pia akaongezea kwamba Ramsdale ambaye alikiri anapitia kipindi kigumu bado Arteta hajamwambia majukumu yake kwa sasa baada ya kupokwa namba.

“Ramsdale atakuwa kipa wa akiba tu, na Raya atakuwa chaguo namba moja labda kitu kitokee, majeraha au kutolewa.”

Ramsdale aliongeza mkataba mpya wa muda mrefu wiki chache kabla ya Raya kusajiliwa kwa mkopo kipindi cha usajili wa kiangazi, huku Ramsdale akikubali uamuzi wa Arteta bila ya kufahamu mambo yatakuwa magumu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live