Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba msuva afungukia dili la mwanae kutua Yanga

Msuva Misri.jpeg Simon Msuva

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba mzazi wa winga wa Taifa Stars, Happy God Msuva amefunguka kuwa dili la Simon Msuva si tu haliwezekani Yanga bali kwa klabu yoyote ya Tanzania.

Mzazi huyo ambaye ni msimamizi wa staa huyo wa zamani wa Yanga, amekiri kusikia mwanae akihusishwa na Yanga lakini anachojua kwa sasa akili yake haipo Tanzania. Arena tunajua Yanga wanasaka saini ya mmoja kati ya Msuva, Mkongomani Macabi Lilepo na George Mpole wa FC Lupopo.

Amesema habari zinazoendelea bado haziendani na malengo makubwa ya mwanae kuendelea kukipiga nje ya nchi na muda wowote kuanza sasa dili likitiki anatimka.

“Mwanangu ananiambia, baba bado nataka kucheza nje ikitokea kucheza hapa nyumbani labda baadae lakini kwa sasa acha nikapammbane huko kwanza,

“Mambo yakikamilika tutaweka wazi lakini wanamichezo wajue sasa hivi Msuva kucheza hapa nyumbani hapana acha akapambane kama ambavyo anahitaji yeye,” alisema baba mzazi wa Msuva.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: