Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba'ke Luis Diaz aangua kilio mwanaye akifunga magoli mawili

Baba'ke Luis Diaz Aangua Kilio Mwanaye Akifunga Magoli Mawili Baba'ke Luis Diaz aangua kilio mwanaye akifunga magoli mawili

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: Radio Jambo

Baba ya mshambulizi Luis Diaz, Luis Manuel Dias Sr alishindwa kujizuia usiku wa kuamkia Ijumaa alipomtazama mwanawe akifunga mabao mawili dhidi ya timu ya taifa ya Brazil na kuipa Colombia ushindi muhimu katika mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia la 2026.

Diaz aliifungia nchi yake mabao mawili ndani ya dakika tatu tu kuelekea robo ya mwisho ya mechi kali dhidi ya Brazil ambao wameorodheshwa katika nafasi ya tatu duniani.

Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Estadio Metropolitano Roberto Melendez mjini Barranquilla, Colombia mwendo wa saa tisa usiku wa kuamkia Ijumaa.

Baba ya Diaz ambaye hivi majuzi alitumia takriban siku kumi na mbili mikononi mwa watekaji nyara alikuwemo uwanjani pampja na maelfu ya mashabiki wengine wakati winga huyo wa Liverpool akiipa nchi yake ushindi nyumbani.

Video ambazo zimesambaa kwenye mtandao ya kijamii zinamuonyesha Bw Manuel Diaz Sr akilia kwa hisia huku akishikiliwa na mashabiki wengine baada ya mwanawe kufunga mabao mawili dhidi ya mlinda lango wa Brazil Allison Becker.

Uwanja mzima ulijaa kelele za kusherehekea huku Bw Manuel akitumia machozi ya furaha kueleza hisia zake.

Baada ya mechi hiyo, Luis Diaz alisema ushindi huo na mabao yake yanamwendea baba yake ambaye alipitia kipindicha kutisha siku chache zilizopita.

"Nilikuwa nikimfikiria baba yangu muda wote uwanjani, kila mara alikuwa na mawazo sahihi katika nyakati ngumu," Luis Diaz aliwaambia waandishi wa habari.

Aliongeza, "Ushindi huu, mabao haya yanaenda kwake."

Chanzo: Radio Jambo