Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba amdai Samatta Tsh 40,000

Samatta Chama Mbwana Samatta

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baba mzazi wa mshambuliaji wa PAOK ya Ugiriki na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta, Mzee Ally Samatta amesema anamdai nyota huyo shilingi elfu 40 kwa kosa la kukosa penati mbili akiwa na klabu yake hiyo.

Mzee Ally Samatta ameweka utaratibu katika suala la upigaji wa penati kwa watoto wake wawili wanaocheza soka, Mbwana Samatta anayecheza barani Ulaya na kaka yake Mohamed Samatta ambaye anacheza nchini Tanzania katika klabu ya Ken Gold FC inayoshiriki Championship.

Kwa Mbwana Samatta anayecheza Ulaya kila akikosa penati moja,anatakiwa kumlipa mzee Ally Samatta Tsh 20,000, na kwa Mohamed Samatta anayecheza Tanzania akikosa penati analipa Tsh 10,000.

Kabla ya michuano ya AFCON 2023 Mbwana Samatta alikosa penati moja akiwa na PAOK na baada ya kurejea katika klabu yake baada ya michuano hiyo, akakosa penati nyingine, hivyo mpaka sasa anadaiwa Tsh 40,000 ambapo Mzee Ally Samatta amesema Mbwana anaujua utaratibu,hivyo akirudi tu Tanzania,atatoa hela hiyo bila hata kukumbushwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live