Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya wingu zito, Mkude ibukia kambini Simba SC

JONAS Kiungo mkabaji wa Simba,Jonas Mkude

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba Jonas Mkude amewasili na kuripoti katika kambi ya Timu ya Simba inayojiandaa kwa msimu ujao.

Klabu ya Simba imethibitisha hilo katika mitandao yake ya kijamii na pia wametoa picha zinazomuonesha kiungo huyo akijiunga na wachezaji wenzake.

Hali hiyo imeibua hisia za wengi hasa ikikumbukwa kuwa kuelekea mwisho wa msimu uliopita,yaani Juni 7,2021 kiungo huyo alikutwa na makosa ya utovu wa nidhamu na kufikishwa katika kamati ya maadili ya Klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wa kamati hiyo Suleiman Kova.

Maamuzi yaliyopitishwa ni kupelekwa hospitali kupimwa kabla ya kuchukuliwa hatua, lakini tangu wakati huo hakuna taarifa yoyote iliyotoka juu ya mchezaji huyo mpaka hii leo alipoonekana na wachezaji wenzake kambini.

Bado haijawekwa wazi kama Mkude atasafiri na timu kwenda Morocco kwa maandalizi ya msimu ujao ama la.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live