Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya usajili wa Szoboszlai Liverpool, Kituo kinachofuata!

Naom 64a0110cecf41 beki wa Sporting Lisbon Gonçalo Inácio

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya usajili wa Dominik Szoboszlai katika kikosi cha Liverpool nafikiri Liverpool tayari wamesha cover maeneo mawili muhimu kwenye kiungo chao

Namba 8 wa upande wa kushoto ( LCM ) Alexis Mac Allister ... ambaye jukumu lake kubwa kwa mfumo mpya wa Liverpool ni kuhakikisha timu inatawala mchezo / umiliki wa mpira lakini pia kusaidia timu kiulinzi pale wakipoteza mpira arudi kuwa karibu na Fabinho na TAA kurejea nafasi ya beki wa kulia

Namba 8 wa kulia ( RCM ) Dominik Szoboszlai , ku overlap pembeni ya Salah pale Egyptian King akiingia ndani kushambulia katikati ya fullback na beki wa kati wa timu pinzani lakini pia kwa ufundi wake wa kupiga pasi atakuwa kwenye halfspace ya kulia na kupiga krosi .

ENEO LILILOBAKI

Nafikiri kama Liverpool wakifanikiwa kumpata beki wa Sporting Lisbon Gonçalo Inácio maana yake Liverpool watakuwa sawa sawa kwenye ule mfumo wao wa 3-2-2-3 nyuma mabeki watatu ( Konate VVD na Inacio ) .

Robertson ni beki mzuri sana lakini nafikiri kwenye mfumo wa kucheza mabeki watatu nyuma unampa tabu tofauti na nguvu yake ilipo ile ya kushambulia zaidi kupanda juu .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live