Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya ndoo, Simba yataka unbeaten WPL

Simba Queens Unbeaten Baada ya ndoo, Simba yataka unbeaten WPL

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) akiwa na mechi mbili mkononi, kocha wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi, amesema taji halitoshi, kwani kiu waliyonayo ni kumaliza msimu bila kupoteza mchezo wowote.

Simba ilitwaa ubingwa huo juzi baada ya kuifunga Alliance Girls mabao 3-0 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, ikirejesha taji hilo ililolipoteza msimu uliopita kwa JKT Queens, huku ukiwa ni ubingwa wa nne kwani ilishatwaa pia 2020, 2021 na 2022.

Mgosi alisema suala la ubingwa limekamilika, lakini malengo hayajatimia kwani wanahitaji kumaliza ligi bila kupoteza mchezo (unbeaten), huku akiwapongeza wachezaji kwa kufuata maelekezo ya benchi la ufundi, kuyafanyia kazi na kuipambania timu kwani ndiyo siri ya mafanikio yao msimu huu.

“Tangu nimekuwepo Simba hili ni suala ambalo linajirudia tumekuwa tukichukua ubingwa tukiwa na mechi mkononi. Kikubwa ni kuwapongeza wachezaji kiu waliyokuwa nayo, kufuata mafundisho na kufanikisha tulichokihitaji msimu huu,” alisema Mgosi na kuongeza;

“Ligi inakwisha lakini tuna mashindano ya Afrika Mashariki tunahitaji kufanya usajili na kupunguza watu, kila mtu lazima acheze ili kitakachofanyika kifanywe kwa uhalisia kwa maana mtu kapewa nafasi kashindwa kuonyesha.”

Nyota huyo wa zamani wa Simba, alisema ubingwa huo ni furaha kwa wanasimba wote, kwani walikuwa na kiu ya kuubeba baada ya timu ya wanaume kuambulia nafasi ya tatu katika Ligi Kuu Bara.

“Ni faraja kwa wapenzi wote wa Simba na tunajivunia,” alisema Mgosi.

Chanzo: Mwanaspoti