Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kuondolewa Kombe la Shirikisho, Biashara UTD watoa ya moyoni

Biashara United Wakiwasili Ethiopia. Baada ya kuondolewa Kombe la Shirikisho, Biashara watoa ya moyoni

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SIKU chache baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, uongozi wa Biashara United umesema ukata umekatisha safari ya mafanikio kwenye mashindano hayo huku wakibainisha kuwa bado wana nafasi ya kushiriki msimu ujao.

Akizungumza na Mwanaspoti, katibu mkuu wa klabu hiyo Haji Mtete alisema walikuwa wamejiandaa kisaikolojia kwa lolote watakalolipata, hivyo haikuwa sapraizi kwao na baada ya kuondolewa kwenye mashindano hayo nguvu zao wanahamishia Ligi Kuu na wana imani watapata nafasi kama hiyo.

Alisema walikuwa na kazi kubwa kuwatuliza wachezaji ambao waliamini mashindano hayo ni moja ya njia yao kujipatia mafanikio, lakini haijawa hivyo kutokana na ukata, hivyo kujikuta wanashindwa kukamilisha walichokuwa wamekipanga.

“Kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa kwa lolote, lakini kwa wachezaji tuliwahakikishia nafasi bado ipo ili waendelee kufanya vizuri kwenye ligi tukiwaambia kuwa ni moja ya maandalizi lakini imekuwa tofauti,” alisema nakuongeza kuwa.

Mtete aliongeza kuwa pamoja na kupata mechi mbili wamejifunza namna ya kujiandaa kwenye ushiriki wa mashindano ya kimataifa..

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz