Matajiri wa zabibu kutoka Dodoma wakifanya mazoezi yao ya mwisho kabla ya kuelekea Morogoro kukabiliana na walima miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar wamesema wamejiandaa kupambana na kusalia Ligi Tanzania Bara.
Hayo yamesemwa na Kassim Liogope, Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji akizungumzia mandalizi yao kuelekea mechi na Mtibwa Sugar kwenye NBC Premier League.
"Matokeo ambayo tumeyapata dhidi ya Azam FC hivi karibuni (Dodoma 1-0 Azam FC) yameisaidia sana timu yetu. Kwanza yametujengea kujiamini, sasa tunakwenda kucheza na timu za level yetu.
"kama tutacheza kama tulivyocheza michezo mwili iliyopita, tunaamini tunakwenda kupata alama tatu Manungu. Tunajua ubora wao na mapungufu yao yapo sehemu gani.
"Ligi sasa inaelekea mwishoni na kila timu imejiandaa. Sisi na Mtibwa hatuendi kugombani kuwa mabingwa, kila mtu anakwenda kugombani asishuke daraja," amesema Liogope.
Beki Hassan Kessy
"Mechi itakuwa ngumu kuliko mechi nyingine, tumetumia nguvu sana katika mchezo uliopita, tumepata matokeo, lakini fainali yetu ipo Morogoro."
Nahodha Mbwana Hamisi 'Kibacha'
"Ligi imefika hatua za mwisho, kila timu inapambana, lakini kikubwa sisi tunahitaji alama tatu. Tunaamini sisi wachezaji kila mchezo tunatakiwa kupambana na kuhakikisha tunapata ushindi ili kuvuka vizuri katika msimamo wa Ligi."