Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kichapo, Kocha Southgate atupa taulo England

Gareth Southgate Kocha Gareth Southgate

Tue, 16 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gareth Southgate ametangaza kujiuzulu kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya England baada ya miaka minane. Chama cha Soka ‘FA’ kilitarajia kumsainisha mkataba mpya baada ya kuiongoza timu hiyo hadi fainali ya Euro 2024, lakini Southgate ameamua kutafuta changamoto mpya.

"Kama raia wa England mwenye fahari, imekuwa heshima ya maisha yangu kuichezea England na kuifundisha kama kocha mkuu," Southgate alisema.

"Imemaanisha kila kitu kwangu, na nimejitolea kwa muda wangu wote. Lakini ni wakati wa mabadiliko. Fainali ya dhidi ya Hispania ilikuwa mchezo wangu wa mwisho kama kocha mkuu wa England.”

Southgate mwenye umri wa miaka 53 ndiye kocha aliyefanikiwa zaidi England katika suala la utendaji thabiti wa mashindano makubwa.

England pia ilitinga fainali ya Euro 2020, ikifungwa na Italia, na nusu fainali ya Kombe la Dunia mnamo 2018, ilipofungwa na Croatia.

Katika Kombe lake lingine la Dunia, timu hiyo ilitolewa na Ufaransa katika robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live