Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kichapo, Azam waanza na hili

Djuma Shaban Azam FC.jpeg Baada ya kichapo, Azam waanza na hili

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuambulia kichapo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, matajiri wa Dar Azam FC wameanza maandalizi.

Ni Mzizima Dabi ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-2 Azam FC ambapo Aziz Ki aliandika rekodi ya kufunga hat trick katika mchezo huo.

Mabao ya Azam FC inayonolewa na Yusuph Dabo yalifungwa na Gibril Sillah na Prince Dube. Ni Oktoba 27 2023 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Namungo FC ipo chini ya Dennis Kitambi ambaye ni kocha msaidizi akiendeleza majukumu ya Cedric Kaze aliyebwaga manyanga.

Timu hiyo ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukisoma Namungo 2-3 Singida Fountain Gate ikayeyusha pointi tatu mazima hivyo inaingia kwenye mchezo huo kwa hesabu kubwa.

Timu zote mbili kwenye mechi zao zilizopita hazikuambulia ushindi na idadi ya mabao waliyofungwa yana mfanano.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live