Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Yanga, Ilanfya sasa aitaka Simba

Ilanfya X Diarra Baada ya Yanga, Ilanfya sasa aitaka Simba

Thu, 26 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unakumbuka kipigo walichopata Yanga kule Mbarali? Sasa unaambiwa yule staa aliyepeleka kilio kwa ‘Wananchi’ anawahitaji Simba kuhakikisha msimu huu anawanyamazisha wote.

Yanga katika mechi sita ilizocheza imepoteza mchezo mmoja ilipokufa kwenye Uwanja wa Highland Estate wilayani Mbarali walipochapwa mabao 2-1 ikiwa ni mwendelezo wa timu hiyo kunyooshwa na Ihefu.

Katika mchezo huo Yanga ndio ilitangulia kupata bao la mapema kupitia kwa Pacome Zouzoua dakika ya nne kabla ya Leny Kisu kusawazisha kisha Charles Ilanfya kupigilia msumari wa mwisho na kuihakikishia Ihefu pointi tatu.

Kwa sasa timu hiyo inajiandaa kuwakabili Simba kwenye muendelezo wa Ligi Kuu raundi ya saba kwao na sita kwa Wekundu, mechi itakayopigwa, Oktoba 28 kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Timu hiyo iliyopo nafasi ya 10 kwa pointi saba inawakabili wapinzani hao waliopo nafasi ya pili kwa alama 15, itakuwa mchezo wa pili kwa kocha mkuu, Moses Basena raia wa Uganda baada ya ule dhidi ya Coastal Union ambao aliambulia sare.

Akizungumza nasi, Ilanfya alisema siyo mara ya kwanza kuwafunga Wekundu hao, hivyo wanaendelea kujipanga kuhakikisha wanapata ushindi.

Alisema pamoja na ratiba kubana lakini anaamini watapambana kutafuta ushindi akibainisha kuwa ugumu utakuwapo kwenye mechi hiyo kutokana na wapinzani walivyo.

“Ratiba ndio haijaeleweka vizuri ila tutapambana kutafuta matokeo mazuri, nimefunga sana Simba, hivyo nikuomba siku hiyo afya njema ili kufanya kile nilichowahi kufanya hata kwa wengine kama Yanga,” alisema nyota huyo aliyewahi kukipiga Msimbazi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: