Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Wembley, Endric atupia tena Santiago Bernabeu

Endrck Vs Spain.jpeg Kinda mpya wa Real Madrid na timu ya taifa Brazil Endrick

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinda mpya wa Real Madrid na timu ya taifa Brazil Endrick mwenye umri wa miaka 17 anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga kwenye viwanja vikubwa viwili mfululizo baada ya jana kuifungia Brazil goli moja kwenye sare ya 3-3 dhidi ya Hispania.

Endrick ambaye alifunga siku tatu zilizopita dhidi ya Uingereza kwenye dimba la Wembley amefunga tena dhidi Hispania kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu, mmoja kati ya viwanja vya nyumbani vya timu ya Taifa ya Hispania unaomilikiwa na klabu ya Real Madrid ambayo pia ni klabu atakayoanza kuitumikia kuanzia msimu ujao.

Kwenye sare hiyo, mabao mengine ya Brazil yalifungwa na Rodrigo na Lucas Paqueta huku ya Hispania yakifungwa na Rodri na Dani Olmo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live