Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Sopu, vita ya Yanga yahamia kwa Sillah

Sillah Mbabe Baada ya Sopu, vita ya Yanga yahamia kwa Sillah

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya Abdul Suleiman Sopu wa Azam FC kuwafunga Yanga mara mbili akiwa na timu tofauti, kwa sasa winga wa timu hiyo Gibril Sillah ndio kiboko ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu na Kombe la Azam (ASFC).

Sopu akiwa na Coastal Union msimu wa 2022/2023, aliifunga Yanga mabao matatu (hat-trick) kwenye fainali ya Kombe la ASFC, ndipo msimu uliofuata akasajiliwa na Azam FC, Desemba 25, alifunga mabao mawili timu yake ilipopoteza kwa mabao 3-2.

Kwa sasa bahati ipo kwa winga mpya, Sillah aliyetua msimu huu akitokea Raja Casablanca ya Morocco ambaye ameshawafunga mabingwa hao mabao mawili na asisti moja.

Juzi Yanga ilipokea kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Azam, kwenye muendelezo wa Ligi Kuu katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kinakuwa kichapo cha pili baada ya Oktoba 04, kupoteza kwa mabao 2-1 ugenini dhidi ya Ihefu Mbeya.

Bao la kwanza la Azam lilifungwa na Sillah akiwa ndiye mchezaji aliyeifunga Yanga nyumbani na ugenini msimu huu wa ligi, huku lile la pili likiwekwa kimiani na nyota wa zamani wa timu hiyo ya Wananchi, Feisal Salum 'Fei Toto'.

Ushindi huu unaifanya Azam isogee hadi nafasi ya pili ya ligi ikiwa na pointi 47 zikiwa ni tano tu nyuma ya vinara Yanga yenye pointi 52 kileleni mwa msimamo wa ligi.

Chanzo: Mwanaspoti