Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Oparesheni, Nado nje msimu mzima

Nado Op.jpeg Kiungo wa Azam FC, Iddi Selemani "Nado" akiwa na timu ya madaktari

Wed, 22 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Azam FC. Iddi Selemani amefanyiwa Oparesheni ya Goti nchini Afrika ya Kusini kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimkabili.

Kwa upasuaji huo, Nado atakosa sehemu yote iliyobaki ya msimu wa Ligi kuu Bara 2021/2022.

Nado aliumia katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar, Novemba 30 mchezo walioibuka na ushindi wa goli 1-0.

Kiungo huyo alipata majeraha ya kukatika mtulinga wa kati (Anterior Cruciate Ligament) wa goti lake la mguu wa kulia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live