Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Onyango kuomba kusepa Simba, mapya yaibuka

Simba Wakwama Arusha.jpeg Baada ya Onyango kuomba kusepa Simba, mapya yaibuka

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Beki kisiki wa Simba, Joash Onyango huenda asionekane tena msimu ujao wa Ligi Kuu Bara baada ya kuuomba uongozi wa timu hiyo kuvunja mkataba wake uliobaki ili aende kujaribu maisha mengine ya soka nje ya Simba.

Beki huyo alitua nchini Agosti 14, 2020 akitokea Gor Mahia ya nchini Kenya akisaini mkataba wa miaka miwili, aliutumikia kwa mafanikio makubwa na baadaye kuongezwa mwaka mmoja unaotarajia kumalizika msimu ujao.

Habari kutoka ndani ya Simba zilieleza kuwa mchezaji huyo kutokana na lawama za mara kwa mara anazopewa kila anapofanya makosa uwanjani ameomba kumalizana nao ili aondoke.

"Wachezaji ni wengi ambao hawana furaha ndani ya Simba, sasa lakini Onyango ameona isiwe shida kwa kuamua kuandika barua ya kuomba kuondoka hilo lipo chini ya viongozi wanalijadili;

"Tunaweza tusiwe naye msimu ujao kwasababu hata viongozi pia walikuwa wanamtafutia sababu ili kumuondoa kikosini, hivyo kwasababu yeye mwenyewe kaomba kuondoka msimu ukiisha utaratibu utafanyika." kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilisema wanatambua mchango wa mchezaji huyo ndani ya Simba na kuamini kuwa mchezo wa soka una vitu vingi hivyo hawana budi kumpa nafasi ya kuondoka ili kuondoa changamoto iliyopo ya kuangushiwa mzigo kila timu inapopata matokeo mabaya.

Alipotafutwa beki huyo ambaye alisema hafahamu taarifa hizo zimetoka wapi kwaupande wake kama mchezaji hawezi kuzungumzia hilo.

"Siwezi kuzungumza chochote kuhusiana na suala hilo kama lipo viongozi ndio watu sahihi wa kulizungumzia lakini mimi siwezi kuwa na jibu kuhusiana na mambo ambayo yamekuwa yakizushwa na watu;

"Tanzania kumekuwa na kawaida ya watu kuandika vitu ambavyo hawana uhakikia navyo na kuvisambaza kama umesikia mitandaoni siwezi kulizungumzia suala hilo na kama lipo watu sahihi wa kulizungumzia ni viongozi." alisema.

Beki huyo tangu ametua nchini ameisaidia timu yake kutwaa taji moja akicheza kwa mafanikio kikosi cha kwanza hadi sasa ni mchezaji ambaye ana uhakika wa kucheza kikosi cha kwanza sambamba na Henock Inonga.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: