Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya Messi, Mbappe hana sababu ya kuondoka - Mwenyekiti PSG

Https  Therealchamps.jpeg Nyota wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe

Thu, 12 Aug 2021 Chanzo: Mwanaspoti

Mwenyekiti wa Paris Saint-Germain (PSG), Nasser al-Khelaifi leo Jumatano amesema Mshambuliaji Kylian Mbappe "hana sababu" ya kuiacha klabu hiyo baada ya kuwasili kwa Lionel Messi, ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili.

Mbappe yuko katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake na amekuwa akihusishwa na mipango ya kuondoka PSG, huku Real Madrid ikionyesha nia ya kumsajili mshambuliaji huyo aliyekuwemo katika kikosi cha Ufaransa kilichotwaa Kombe la Dunia.

"Kylian ni mkazi wa Paris, ni mshindani sana. Alisema alitaka timu yenye ushindani," alisema Al-Khelaifi.

"Kwa sasa hakuna aliye na ushindani zaidi yetu. Hana sababu ya kufanya lolote jingine, zaidi ya kubakia", aliongeza.

Mwezi Mei, mshambuliaji huyo mwenye miaka 22 aliiambia Canal Plus kuwa anataka kuwa sehemu ambako "anaweza hasa kushinda, ambako kuna mpango mzito."

Mbappe bado hajasaini Mkataba Mpya na klabu hiyo ya Parc de Princes, tofauti na Neymar, ambaye hivi karibuni alikubaliana mkataba ambao utambakiza PSG hadi mwaka 2025.

Chanzo: Mwanaspoti