Baada ya aliekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Simba SC, kukemea kitendo cha CEO wa Simba kuzuiliwa kuingia uwanjani siku ya Jana jumamosi Disemba 11 kushuhudia mpambano wa Watani wa Jadi kati ya Simba na Yanga.
Viongozi na Vigogo mbalimbali kutoka ndani ya klabu ya Simba wameendelea kutoa matamko kkulaani kitendo hicho.
Safari hii ni Aliewahi kuwa mtendaji Mkuu wa Simba SC, Crescentius Magori ambae kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa 'Twitter" amelaani kitendo hicho.
Magori ameandika;
Pole kwa M/kiti wa bodi na CEO kwa yaliyotokea jana. Yatupasa tuseme No kwa vitendo, Vitendo hivi viwe chachu ya kuanza Bunju development leo! Rais, M/kiti wa Simba, M/kiti wa bodi, Bodi nzima na CEO tufanye maamuzi magumu! Simba tukiamua hatushindwi! #NguvuMoja
TFF kupitia taarifa yake iliyotoka jana mara tu baada ya mchezo na kueleza sababu hasa za Babra kuzuiliwa uingia eneo la VVIP, ni kutokana na watoto kutoruhusiwa eneo hilo.