Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baaca afunguka kupishana na Diarra uwanjani

Baaca Na Diarra Uwanjani Baaca afunguka kupishana na Diarra uwanjani

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Kikosi cha Yanga, Ibrahim Hamad Bacca amefunguka baada ya kuonekana kutoelewana na golikipa wake Djiguo Diarra wakati wa mchezo dhidi ya Ihefu, jana Jumatatu, Machi 11, 2024.

Katika mchezo huo ambao Yanga waliibua na ushindi wa mabao 5-0 katika Dimba la Azam Complex, Chamazi, kuna wakati Bacca na Diarra walikuwa kwenye hali ya kutokuelewana baada ya kipa huyo kumfuata beki wake na kutaka kuucheza lakini Bacca aliung'ang'ania mguuni jambo ambalo lilionekana kama kumkera Mdaka Mishale.

“Kuna muda mimi na Diarra tulishindwa kuelewana kila mtu anautaka mpira, hii ni kutokana na uchu wa umakini kwenye idara ya ulinzi kwa sababu ilikuwa moyoni mwetu.

“Tunafarijika kuona kwamba tunaondoka na clean sheet kwa sababu sisi kama mabeki ushindi wetu ni cleansheet ukiacha ushindi wa timu. Tunajivunia kupata clean sheet kwa mechi kama hizi,” amesema Bacca.

Itakumbukwa kuwa, Ihefu ndiyo timu iliyofungwa na Yanga bao 2-1 msimu uliopita na kuiharibu unbeaten yao ya 49 kuelekea 50.

Msimu huu, Ihefu ndiyo timu pekee ambayo imeifunga Yanga kwenye michezo yake yote 18 ambayo imecheza, hivyo Wananchi walikuwa na kila sababu ya kulipa kisasi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: