Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Yanga wamtambulisha Bernard Morisson

Bernard Morisson Yanga Tena.jpeg Bernard Morisson amerudi tena Jangwani

Sun, 3 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hayawi hayawi sasa yamekua. Baada ya sintofahamu kwa majuma kadhaa hatimaye Yanga wamekata mzizi wa fitina baada ya usiku huu kumtambulisha raia wa Ghana, Bernard Morisson kujiunga nao akitokea kwa mahasimu wao Simba SC.

Morisson aliekuwa Yanga hapo awali aliondoka na kujiunga na Simba kwa mkataba wa miaka miwili , mkataba ambao unaisha Agosti 14 mwaka huu.

Tayari Yanga wameanza kuimarisha kikosi chao baada ya kumaliza msimu kwa mafanikio makubwa wakifanikiwa kubeba mataji matatu msimu wa 2021/2022.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live