Uongozi wa Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kumwajiri Ouanane Sellami (42) raia wa Tunisia kuwa Kocha Msaidizi kwa Mkataba wa miaka miwili.
Sellami ni mapendekezo ya Kocha Mkuu Roberto Oliviera "Robertinho" ambapo ataungana na Juma Mgunda kuongoza benchi la Ufundi.
Sellami ana Shahada ya Uzamili ya Elimu ya Viungo ya Michezo kutoka Taasisi ya Superieur Education Sportive Sfax ya nchini Tunisia.
Sellami ana leseni B ya CAF na kabla ya kujiunga na Simba alikuwa akiifundisha Timu ya Almadina ya Libya kwa mwaka 2022.
Ujio wa Sellami Msimbazi ni kwa lengo la kuliongezea nguvu benchi la Ufundi kwa ajili ya michuano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Afrika.