Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Simba washusha chuma kingine hatari, rekodi zake usipime!

Simba Washusha Mashine Mpya #BREAKING: Simba washusha chuma kingine hatari, rekodi zake usipime!

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Simba SC wametangaza kumsajili mlinzi wa kati Che Malone, kutoka nchini Cameroon kwa mkataba wa miaka mitatu.

Kupitia Simba App, Simba wamesema wanaamini uzoefu wa mlinzi huyo wa kati katika michuano ya Kimataifa unakwenda kuongeza nguvu katika kikosi chao msimu ujao 2023-24.

Malone amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Cotton Sports kilichotwaa ubingwa wa Ligi Kuu wa Cameroon msimu uliopita akiwa nahodha akicheza mechi karibu zote.

Malone ambaye anajulikana kwa jina la utani la Ukuta wa Yericko ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu nchini Cameroon (MVP) msimu wa 2022-23.

Kama hiyo haitoshi, Malone ameitwa kwenye timu ya Taifa ya Cameroon (Indomitable Lions) pamoja na timu inayoshiriki michuano ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).

Malone anakuwa mchezaji wa tatu wa kutambulishwa kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi baada ya Willy Onana na Aubin Kramo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live