Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Simba Yamtimua Pablo, Kocha wa Viungo

Pablo Kwa Heriii Simba yaachana na Pablo na Daniel De Castro Reyes

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Msimu mbaya wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho kwa msimu wa 2021/2022, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Klabu ya Simba Sports Club imevunja Mkataba na Kocha Mkuu wa Kikosi hicho Mhispaniola Pablo Franco na Kocha wa Viungo Daniel De Castro Reyes.

Katika Taarifa Rasmi iliyotolewa na Klabu ya Simba katika Mitandao yake ya Kijamii, leo Mei 31 imewashukuru walimu hao kwa michango yao wakati wa utumishi wao ndani ya Klabu.

Pablo aliwasili rasmi nchini Novemba 10, na amedumu ndani ya Kikosi cha Simba kwa miezi sita tu.

Pablo ameifikisha Simba SC Robo Fainali mbili, ambazo ni ile ya Kombe la Shirikisho Afrika na Kombe la Azam Sports Federation.

Soma kwa Kirefu hapa chini, Taarifa ya Klabu ya Simba;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live