Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Meneja wa New Castle ang'atuka

FCIjoK9X0AArsFF Steve Bruce, Meneja alieachia ngazi

Wed, 20 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa New Castle United, Steve Bruce ameachia ngazi ndani ya Klabu hiyo baada ya makubaliano ya pande zote.

Katika taarifa yake rasmi, Klabu ya New Castle imesema, Graeme Jones atakuwa Mwalimu wa mpito na ataanza na mechi yao dhidi ya Crystal Palace mwishoni mwa wiki.

Steve Bruce anaondoka ikiwa ni siku 13 tu, tangu klabu hiyo inunuliwe na kuwa chini ya wamiliki wapya waotoka Falme za kiarabu.

Tetesi zinadai kipigo cha magoli 3-2 walichokipata kutoka kwa Tottenham ndicho kilichoharakisha kuondolewa kwa kocha huyo.

Kazi ya kumsaka Mwalimu mpya inaendelea huku Antonio Conte, Steven Gerrard wakipigiwa chapuo kushikilia wadhifa huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live