Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Karim Benzema atangaza kustaafu Ufaransa

Benzema G9foazwx3wtx121v132kuv82z Karim Benzema

Mon, 19 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Klabu ya Real Madrid, Karim Benzema ametangaza kustaafu kuitumikia Timu yake ya Taifa ya Ufaransa akiwa na umri wa miaka 35.

Benzema ametangaza uamuzi huo siku moja tu baada ya kumalizika kwa Michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Qatar, na kuona Argentina wakiibuka Mabingwa.

Benzema alijumuishwa kwenye kikosi cha Ufaransa lakini hakucheza hata mchezo mmoja baada ya kupata majeraha siku moja kabla ya kuanza kwa michuano hiyo.

Akitangaza uamuzi wake huo katika siku yake ya kuzaliwa Benzema ameandika;

“Nimefanya juhudi na makosa ambayo ilinichukua kuwa hapa nilipo na ninajivunia,” Karim Benzema".

Benzema anastaafu Timu ya Taifa ya Ufaransa akiwa mfungaji bora namba tano akiwa amepachika magoli 37 katika michezo 97 aliyoichezea Ufarnsa kati ya mwaka 2007 mpaka 2022.

Alikosekana kwa kipindi kirefu Timu ya Taifa ya Ufaransa kwa skendo ya kumrekodi mchezaji mwenzake mkanda wa ngono ikiwemo fainali za Mwaka 2018 nchini Urusi ambako Ufaransa waliibuka Mabingwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live