Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

#BREAKING: Chelsea wamtimua Thomas Tuchel

Tuchel Thomas Tt.jpeg Kocha Thomas Tuchel

Wed, 7 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la London, Kalabu ya Chelsea wamemtimua Kocha wao Mjerumani Thomas Tuchel baada ya kuiongoza timu hiyo katika michezo saba tu msimu huu.

Kufukuzwa kwa Tuchel kumekuja kufuatia kipigo cha jana usiku cha goli 1-0 kutoka kwa Dinamo Zagreb mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Katika taarifa yake rasmi klabu ya Chelsea imesema;

"Benchi la ufundi la Chelsea kwa sasa litachukua majukumu yote ya kusimamia mazoezi na matayarisho kuelekea michezo inayofuata wakati klabu ikijiandaa kumtangaza Kocha mpya"

Tuchel alijiunga na Chelsea January 2021, na kuanza kazi katika klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ikiwemo kubeba taji la Ligi ya Mabingwa msimu wa kwanza klabuni hapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live