Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BREAKING: Antonio Conte kocha mpya Spurs

Conte New Coach Antonio Conte, ameteuliwa kuwa Kocha mpya Spurs

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Tottenham imemtangaza kocha wa zamani wa Chelsea na Inter Milan, Antonio Conte kuwa kocha wake mpya.

Klabu hiyo ya ligi kuu England, ilimtimua Nuno Espirito Santo siku ya Jumatatu baada ya michezo 17 tu, huku timu hiyo ikishika nafasi 8 kwenye msimamo wa EPL.

Conte anarejea London baada ya kushinda taji la ligi kuu katika msimu wake wa kwanza akiwa na Chelsea mwaka (2016-17) , akatwaa FA Cup katika msimu wake wa pili kabla ya kutimuliwa mwaka 2018.

Muitalia huyo, mwenye miaka 52, baadae akaiongoza Inter Milan kutwaa taji lao la kwanza la ligi kuu ya Italia, Serie A katika miaka 11 kabla ya kuondoka klabuni hapo mwezi Mei mwaka huu.

Conte aliiongoza Inter kwa miaka miwili na Inter wenyewe walisema walikubaliana kusitisha mkataba wake ambao ulisalia na mwaka mmoja.

Kocha huyo wa zamani wa Juventus na timu ya taifa ya Italia alianza mazungumzo na Tottenham katika majira ya joto ili kumrithi aliyekuwa kocha wa Spurs wakati huo, Jose Mourinho, lakini mazungumzo yalikwama, kabla ya Spurs kuamua kumuajiri kocha wa zamani wa Wolves mwishoni mwa mwezi Juni, ambapo Mreno huyo, amedumu kwa miezi minne tu na Spurs.

Conte amesaini mkataba mpaka majira ya Joto mwaka 2023, kukiwa na kipengele cha kuongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live