Kikosi cha Yanga leo Alhamisi, Januari 19, 2023 jioni kimeendelea na mazoezi jioni kwenye uwanja wa Avic, Kigamboni Dar es Salaam kwa kucheza mechi ya mazoezi na timu ya Dar City.
Kwenye mchezo huo uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0, ulitumiwa kwa benchi letu la ufundi kutoa nafasi kwa wachezaji wote waliorejea kambini.
Bao pekee la Yanga limefungwa na mshambuliaji mpya kutoka Zambia Kennedy Musonda.
Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa, nyota wa Yanga waliorejea kwenye mazoezi leo ni kiungo Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso, winga Benard Morrison raia wa Ghana na kiungo Yanick Bangala wa Congo DR waliokuwa mapumzikoni.
Wachezaji ambao hawajaripoti kambini mpaka sasa ni Feisal Salum na beki Mamadou Doumbia.
Aidha, kikosi hicho kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu, dhidi ya Ruvu Shooting, utakaochezwa Jumatatu, saa 1:00 usiku katika dimba la Benjamin Mkapa.
Katika mchezo huo,kikosi kilichoanza ni;
Kipindi cha kwanza
Kikosi ambacho kilianza
1.Djigui Diarra
2.Kibwana Shomari
3.Lomalisa Mutambala
4.Abdallag Shaibu
5.Bakqri Mwamnyeto
6.Mudathir Yahaya
7.Crispin Ngushi
8.Salum Abubakari Sureboy
9.Kennedy Musonda
10.Clement Mzize
11.Dickson Ambundo.
Kipindi cha pili
1.Metacha Mnyata
2.Djuma Shabani
3.Dqvid Bryson
4.Ibrahim Bacca
5.Dickson Job
6.Kibwana Shomari
7.Jesus Moloko
8.Gael Bigirimana
9.Kennedy Musonda
10.Clement Mzize
11.Farid Mussa.