Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki yupo... Fei kaa palee

Aziz Ki X Mayele Aziz Ki yupo... Fei kaa palee

Thu, 5 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kuna mastaa Simba, Yanga na Azam FC ambao wakikosekana timu zao zinaweza kujikuta kwenye wakati mgumu wa kupata matokeo ya ushindi na hata zikishinda unakuwa ushindi kiduchu, lakini Aziz Ki ameonekana kuwasahaulisha mashabiki wa Yanga uwepo wa Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwenye timu hiyo.

Tegemeo la Yanga kwenye kufunga ni straika Fiston Mayele mwenye mabao 14, wakati anayemfuatia ni kiungo mshambuliaji Fei Toto aliyeachana na timu hiyo hivi karibuni, ingawa Aziz Ki, anakuja kwa kasi na sasa ana mabao manne, huku akionekana kumudu zaidi akicheza namba 10 kuliko namba nyingine uwanjani na ubora wake ukiongezeka zaidi baada ya Fei kuondoka.

Aziz Ki, mechi alizocheza namba 10, baada ya Fei Toto kuondoka Yanga, alichangia ushindi wa mabao 3-2, dhidi ya Azam FC, bao la Yanga la kusawazisha mpira ulianzia kwake akatoa pasi kwa Bernard Morrison aliyempa asisti ya bao Mayele dakika ya 31, Ki alifunga bao la pili dakika ya 32 na dakika ya 77 Ki alipiga mpira wa kutenga na Farid Mussa kufunga bao la tatu.

Kwa ujumla kwenye mechi 15 alizocheza Ki, amefunga mabao manne, baadhi ya mechi ni Simba, Azam FC na Mtibwa Sugar, pia ametoa asisti tatu, wakati Fei katika mechi 16 alifunga mabao sita na pasi za mabao mbili, hali hii inaonyesha kuwa kama Ki atacheza michezo michache ijayo mbele anaweza kumaliza kabisa ufalme wa Fei Yanga.

Katika mabao 37 ya Yanga Mayele, Ki na Fei Toto wamechangia 27, huku Mayele akichangia asilimia 40, zilizobakia ni za mastaa wengine wa timu hiyo.

Lakini hakuna shaka kuwa, baada ya kuondoka kwa Fei ubora wa Ki umeonekana maradufu, lakini naye uwanjani amekuwa akijituma zaidi na kuwaonyesha mashabiki wa Yanga kuwa anaweza kufanya mambo makubwa hata bila Fei kuwepo.

SIMBA

Simba inamiliki mabao 47, katika hayo Clatous Chama amechangia zaidi ana asisti 11 na mabao matatu, sawa na mabao 14 na kuna mechi alikuwa akikosekana timu ilikuwa inapata wakati mgumu kupata ushindi,hali inaweza kuwa tofauti sasa baada ya timu hiyo kumsajili Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.

Ujio wa’Saido’ ndani ya kikosi hicho ambaye ana asisti saba, moja akiipata Simba na mabao matatu dhidi ya Prisons, timu yake mpya ikishinda jumla ya mabao 7-1 Uwanja wa Benjamin Mkapa unaweza kuwa na faida Simba.

Saido wakati yupo Geita Gold alikuwa na asisti sita na mabao manne, hivyo kujiunga kwake Simba kutainufaisha timu hiyo akikosekana Chama anaweza akaokoa jahazi kwa kutengeneza mashambulizi na kufunga.

Mbali Chama na Saido, kuna Moses Phiri ambaye katika mabao 47 ya Simba kachangia 10, sawa na asilimia 21, huku nahodha John Bocco akiwa na mabao tisa sawa na asilimia 20, hivyo akikosekana mmoja wapo mwingine anaibeba timu.

AZAM FC

Kwa upande wa Azam FC, ina mabao 24 anayeongoza kwa idadi kubwa ya mabao ni Idris Mbombo ana saba, anayefutia ni Prince Dube matano na Abdul Sopu manne, ambao watatu hao wamechangia mabao 16.

Chanzo: Mwanaspoti