Mjadala mkubwa baina ya kiungo wa Simba SC, Clatous Chama na kiungo wa Yanga SC, Aziz Ki yupi ni bora unaendelea kama ulivyoanza.
Wote ni namba 10 yaani viungo washambuliaji wakiwa na sifa ambazo zinatofautiana. Lakini kuna vitu Azizi Ki anaonyesha kuwa anamzidi Clatous Chota Chama haswa katika kupiga mashuti makali na kufunga mabao.
Mashuti makali yameamua katika mechi dhidi ya Simba,Azam FC,Club African na mechi nyingine. Tofauti na Chama ambaye anategemea zaidi mabao ya Curving (mzungusho) ambayo pia Azizi Ki anaweza kuyafunga.
Kwa upande wa kuchezesha timu wote wapo sawa japo Azizi Ki anaweza kupiga pasi ndefu tofauti na Chama ambaye hana usahihi sana kwenye Long Passses.
Bado mjadala unaaendelea lakini kwa sasa Azizi Ki ndiye namba 10 bora kuliko wote kwenye ligi yetu.
Mpaka sasa Aziz Ki ndiye mfungaji bora akiwa na mabao 6 ukiwa ni mzunguko wa 6 wa ligi kuu na kama atapata kucheza bila majeraha nayaona mabao 15 kwa Aziz Ki.