Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki kuzungumza na Wananchi leo

Aziz Ki Mwe Aziz Ki kuzungumza na Wananchi leo

Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Stephane Aziz Ki leo Julai 10, 2024 majira ya saa 8 mchana atazungumza na mashabiki wa klabu hiyo 'Wananchi' kupitia mitandao ya kijamii ya Yanga.

Taarifa hiyo imetolewa na Idara ya habari na mawasiliano ya Yanga huku kukiwa na sintofahamu kuhusu hatma yake hasa baada ya kauli ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye alikiri kuwa nyota huyo hakuwa amesaini mkataba.

Hata hivyo jana katika mahojiano mengine aliyofanya Afrika Kusini, Injinia Hersi alisema majadiliano yalikuwa katika hatua za mwisho na kuwa hatma ya Aziz Ki ingefahamika baada ya saa chache.

Bila shaka kupitia mazungumzo hayo, Aziz Ki ataweka bayana kama ameongeza mkataba au la?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live