Kiungo wa Yanga SC, Stephen Aziz Ki yupo nchini Ufaransa na timu yake ya taifa ya Burkina Faso wakitarajiwa kucheza na timu ya taifa ya Morocco ambao mchezo ulishindwa kufanyika kutoka na majanga ya mji wa Marrakech kikubwa na tetemeko la Ardhi.
Kupitia Msemaji wa Yanga SC, Ally Kamwe amesema kiungo mshambuliaji wao kutoka Burkina Faso anatarajiwa kujiunga na wenzake nchini Rwanda kuwakabili Al-Merreikh.
Yanga wanatarajia kuondoka keshokutwa Alhamisi, Septemba 14, 2023 kuelekea nchini Rwanda ambako watacheza mchezo wa kwanza wa hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AL-Merrikh ya Sudan.