Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki kufanyiwa vipimo leo

Aziz Ki Sta Aziz Ki kufanyiwa vipimo leo

Sat, 28 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Stephane Aziz Ki, leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi ili kufahamu ukubwa wa jeraha lake.

Aziz Ki aliumia sehemu ya chini ya mguu katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Fountain Gate uliochezwa jana Ijumaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kiungo huyo katika mchezo huo, alitolewa uwanjani kipindi cha pili na nafasi yake ikachukuliwa na Clement Mzize.

“Aziz Ki aliumia sehemu ya chini ya mguu, tunakwenda kumfanyia vipimo leo kupata taarifa kamili ya ukubwa wa jeraha lake,” alisema Daktari wa Yanga, Moses Etutu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live