Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki aweka rekodi Sauzi, Yanga waitwa

Aziz Ki Kaizer Aziz Ki aweka rekodi Sauzi, Yanga waitwa

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Kiungo Mshambuliaji wao, Stephane Aziz Ki, aking'ara vilivyo katika mechi ya Kombe la Toyota dhidi ya Kaizer Chiefs, iliyopigwa juzi katika Uwanja wa Bloemfontein, Afrika Kusini na Yanga kubeba taji hilo, mashabiki na wanachama wa klabu hiyo wameitwa kushuhudia makubwa zaidi watakapoivaa Red Arrows ya Zambia Siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi Agosti 4, mwaka huu.

Katika mechi hiyo ya Kombe la Toyota iliyopigwa juzi kwenye Uwanja wa Bloemfontein, Afrika Kusini, Yanga ilishinda mabao 4-0 mawili yakifungwa na Aziz Ki, Mzimbabwe aliyejiunga msimu huu akitokea Azam FC, Prince Dube, na straika wa Kitanzania, Clement Mzize.

Baada ya mechi hiyo, Aziz Ki, alikabidhia hundi ya Rand 5,000 (sawa na Shilingi 752,804 za Tanzania), ikiwa ni zawadi ya Mchezaji Bora wa mechi ya hiyo.

Katika hatua nyingine jana, Yanga ilitangaza rasmi kuwa siku ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Mabingwa wa Dar Port Kagame Cup, Red Arrows ya Zambia.

Wakizungumza jana Makao Makuu ya klabu hiyo, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, aliyeambatana na Haji Manara ambaye alianza kwa kusema ubora wa Wazambia hao ndio sababu ya kuwaalika kwenye tamasha hilo, hivyo kuwataka mashabiki wa timu hiyo kutoikosa mechi hiyo.

"Habari njema Wanayanga na Watanzania wote, ratiba yetu ya Kilele cha Wiki ya Mwananchi, tutacheza na Red Arrows, ambao wametoka kuchukua ubingwa wa Kagame Cup siku chache zilizopita," alisema Manara.

Aidha, alisema mashabiki wa klabu hiyo hakuna haja ya kukaa nyumbani bali wajitokeze kwa wingi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia timu yao.

"Unakaaje nyumbani na kuacha kuja kuangalia timu yako ambayo katika mechi tatu tu za 'pre season' wametwaa ubingwa huko Afrika Kusini?", alisema Manara.

Manara, alisema kumeandaliwa 'sapraizi' kubwa kwenye utambulisho wa wachezaji wao siku hiyo ya Kilele cha Wiki ya Wananchi.

Kwa upande wa Kamwe, alisema wameandaa ratiba kamili kuelekea kilele cha wiki hiyo ambapo kwa kuanzia usiku wa kuamkia leo watajitokeza uwanja wa ndege kuipokea timu yao ikitokea Afrika Kusini.

Alisema baada ya kuwasili uwanja wa ndege, wameandaa 'parade' kuelekea makao makuu ya klabu hiyo huku wakiwa na kombe la ubingwa wa mashindao ya Toyota walilolitwaa juzi Afrika Kusini kwa kuifunga Kaizer Chief mabao 4-0.

"Pia tumeandaa "jogging" Jumamosi asubuhi, tutafanya mazoezi pamoja na baadaye tutakunywa supu ya pamoja hapa klabuni," alisema Kamwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: