Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki awapania Waarabu

Aziz Ki Vs Azam FC Leo Aziz Ki awapania Waarabu

Thu, 22 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yanga juzi usiku iliendeleza moto kwenye michuano ya Kombe la ASFC kwa kuifumua Polisi Tanzania mabao 5-0, licha ya kupumzisha mastaa wengi wa kikosi cha kwanza na imebainika, Stephane Aziz KI akiiomba mechi hiyo ili kujiweka fiti zaidi kabla ya kuwavaa CR Belouizdad keshokutwa Jumamosi Kwa Mkapa.

Inaelezwa kuwa, Aziz Ki mwenye mabao 10 katika Ligi Kuu akiwa ndiye kinara, alimuomba kocha Miguel Gamondi kumpa nafasi kwa muda mrefu kabla ya kumpisha Shekhan Ibrahim kipindi cha pili katika mechi hiyo iliyopigwa Azam Complex na Yanga kusonga mbele ikitinga 16 Bora, ili ajiweke vizuri kabla ya kuwakabili Waalgeria waliowafumua 3-0 katika mechi ya kwanza ya Kundi D ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayopigwa Jumamosi.

Ipo hivi. Licha ya kocha Gamondi kupumzisha mastaa wa kikosi cha kwanza kuanzia kipa hadi beki timu yake iliyocheza ilipambana na kufunga mabao 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania, lakini Aziz Ki alitumika kwa dakika 68 na ndipo ikabainika aliomba mwenyewe kwa kocha huyo kujitafuta mapema kabla ya kuwavaa Belouizdad.

Akizungumza na Mwanaspoti, Aziz KI aliyetoka kwenye fainali za Afcon 2023 zilizofanyika Ivory Coast, alisema alimuomba kocha mapema nafasi hiyo kwa kazi maalumu.

“Nilichelewa kujiunga na timu baada ya kutoka Afcon tukitolewa hatua na 16 Bora, hivyo bado mwili haujafunguka ndio maana nilimuomba kocha kunipa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ili niendelee kujitafuta,” alisema Aziz Ki.

Aziz Ki, aliyekosekana mechi tatu za ligi dhidi ya Kagera Sugar, Dodoma Jiji na Mashujaa, alisema: “Ukiangalia jana (juzi) wachezaji wengi waliopata nafasi ya kucheza hawana uhakika wa namba ya kucheza mara kwa mara kikosini, lakini walikuwa bora na walikuwa wanayataka matokeo mazuri tuliyoyapata.”

Kwenye mechi tatu alizokosekana Aziz Ki, Yanga ilianza na Kagera Sugar ugenini na kutoka suluhu kisha ikashinda 1-0 kwa Dodoma Jiji, ikaifunga Mashujaa mabao 2-1, ndipo akacheza dhidi ya Tanzania Prisons wakati Yanga ikishinda 2-1 na KMC mjini Morogoro pale Yanga iliposhinda 3-0, lakini mechi zote akitumika kwa dakika chache.

Kiungo huyo kinara wa upachikaji wa mabao msimu huu hadi sasa akiingia kambani mara 10 akizungumzia mchezo wa Jumamosi, alisema hawatarajii mteremko wanajiandaa kushindana ili kufikia malengo.

“Kipimo kizuri kwa timu ni matokeo mazuri lakini ili kupata hayo matokeo tunatakiwa kupambana Jumamosi. Tuna mchezo mgumu ambao tunauchukulia kama fainali tutapambana kuhakikisha tunaipa timu matokeo mazuri.” alisema.

Wakati Aziz KI akiyasema hayo Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi amechekelea kiwango chaker akisema mechi hiyo ilikuwa sehemu ya kumuandaa kiungo huyo kuelekea ile mechi ya Belouizdad.

Gamondi alisema mbali na Aziz KI pia amefurahia kuanza kufunga kwa mshambuliaji mpya, Joseph Guede ambaye alifunga mara mbili kwenye ushindi dhidi ya Polisi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: