Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki atua Dar kuiwahi Al Hilal

Aziz Ki Pic Data (1) Aziz Ki atua Dar kuiwahi Al Hilal

Wed, 5 Oct 2022 Chanzo: Mwananchi

Aziz Ki alikwama nchini Morocco kufuatia kugundulika kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 akiwa katika vipimo vya mwisho kuondoka nchini humo alipokwenda kuitumikia katika michezo miwili ya kirafiki iliyokuwa kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Baada ya kuzuiliwa kwa siku kadhaa nchini humo mshambuliaji huyo alikuja kufanyiwa tena vipimo ili kuangalia maendeleo yake na vipimo kuonyesha hana maambukizi ndipo aliporuhusiwa na mamlaka hiyo.

Yanga inarudi mazoezini kesho huku ikieleza kuwa Aziz Ki atakuwa mmoja wa wachezaji watakaoingia kambini tayari kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Hilal ya Sudan baada ya kuonekana yuko fiti licha ya matokeo ya vipimo hivyo.

Yanga itakuwa Uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa Oktoba 8, 2022 kuwakaribisha Al Hilal katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kurejea kwa Aziz Ki Kutawashusha presha mashabiki wa Yanga ambao waliingia na wasiwasi katika kumkosa mshambuliaji huyo katika mechi hiyo muhimu.

Related Aziz Ki akutwa na Covid Morocco Aziz KI ana jambo lake, apania kuweka rekodi Nabi achekelea Aziz Ki kuitwa Burkina Faso.

Chanzo: Mwananchi