Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki ataka mabao tu Yanga

Stephen Aziz Ki Goals Kiungo Mshambuiaji wa Yanga Azizi KI

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuiaji wa Yanga Azizi KI amesema kuwa anapenda kufunga ama kutengeneza nafasi za mabao akiwa ndani ya uwanja.

Nyota huyo ni ingizo jipya ndani ya Yanga ambapo alijiunga na kikosi hicho akitokea ASEC Mimosas.

Oktoba 23,2022 alifunga bao la pili ndani ya ligi ambapo alimtungua Aishi Manula kwa pigo la faulo akiwa nje ya 18.

Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuwafanya wagawane pointi moja moja.

Nyota huyo amesema:”Ninapenda kufunga na kutengeneza nafasi za mabao nina amini kwamba mashabiki wanapenda kuona haya yanatokea.

“Kikubwa ni ushirikiano na kila mmoja anafanya kazi yake kutimiza majukumu yake hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live