Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki asepa Yanga

Aziz Ki Pic Data (1) Stephane Aziz Ki

Fri, 11 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mfungaji wa bao lililowavusha Yanga kwenye hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika, Stephen Aziz Ki hajarudi na wenzake kwa ruhusa maalum ya uongozi.

Nyota huyo amepewa ruhusa ya kwenda kwao Ivory Coast baada ya kufungiwa michezo mitatu ya ligi.

Yanga wametua mchana huu kutoka Tunisia kupitia Dubai na wanatarajia kwenda Mwanza leo saa moja usiku tayari kwa mchezo wa Jumapili dhidi ya Kagera Sugar.

Wachezaji wote wamerudi isipokuwa Aziz Ki ambaye hadi kocha Nabi anamalizia msafara wao hakuonekana na kuibua shangwe za mashabiki wakihoji mchezaji huyo yupo wapi?

Aziz Ki amefungiwa mechi tatu na faini laki tano kwa kosa kutosalimiana na wachezaji wenzake kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.

Hivyo staa huyo hatakuwa miongoni mwa wachezaji na benchi la ufundi wanaoanza safari usiku wa leo kwaajili ya mchezo wa ligi huko Mwanza.

Chanzo: Mwanaspoti