Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki arejea kuivaa Prisons

Aziz KI Mpira Aziz Ki arejea kuivaa Prisons

Fri, 9 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki tayari amerejea nchini na yupo tayari kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons.

Aziz Ki amerejea kutoka kwenye majukumu ya Timu ya Taifa ya Burkina Faso iliyokuwa ikishiriki michuano ya AFCON nchini Ivory Coast na kuishia hatua ya 16 bora.

Kiungo huyo ndiye kinara wa magoli katika Ligi Kuu ya NBC msimu huu akiwa amefunga magoli 10.

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuvaana na Prisons Jumapili ya Februari 11, 2024 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Mchezo huo utachezwa siku ambayo klabu yetu itakuwa inasherehekea kutimiza miaka 89 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1935.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: