Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki anasepa bure

Aziz Kii WA0006 Aziz Ki

Sat, 25 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

YA AZIZ KI NA HISTORIA YA 'TRANSFER' ZAKE:

Tarehe 30 June, 2024 ndipo Mkataba wa kiungo mshambuliaji wa Yanga kutoka Burkina Faso, Aziz Ki utafikia tamati ikimaanisha umebaki mwezi mmoja pekee.

Kwa mujibu wa taratibu za soka ni kwamba mchezaji akibakiza chini ya miezi 6 kwenye Mkataba wake, anayo ruhusa ya kufanya mazungumzo ya usajili na club yoyote itakayovutiwa naye hivyo kwa sasa Aziz yuko sokoni.

Inavyoonekana wakala wa Aziz Ki ni mjanja kupindukia kwenye suala la biashara kwani kwa mujibu wa mtandao wa Transfer market ni kwamba tangu mwaka 2015 Aziz hajawahi kuuzwa kutoka club alizozipitia.

Kama inavyoonekana pichani; Uhamisho wowote uliofanyika ulikuwa ni huru yaani anasubiri Mkataba ukiisha anasepa na hakai na timu zaidi ya misimu miwili.

Kwa maana hiyo ni dhahiri huwa anatengeneza hela yeye binafsi kuliko kuwanufaisha waajiri wake kumuuza ukizingatia kwa kiwango chake si mchezaji wa kuondoka Bure hata kidogo.

Viongozi wa Yanga kama watahitaji biashara basi watatakiwa kulitazama hili kwa kina ingawa kwa sasa inawezekana ikawa ni 'too late'.

Kuna watu wamesema wanamtazama kwa jicho la uchu, acha tusubiri tuone hili jambo litaishaje.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live