Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki anamvuruga Fei Toto?

Fei Toto Amfunika Aziz Ki Ligi Kuu Fei Toto

Sat, 11 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nimelirudia zaidi ya mara tatu tukio la mkwaju wa penati alioukosa Feisal Salum kwenye mechi dhidi ya Simba na tumepata ABC za kile kilichomtokea kwa kuikosa ile penati ambapo huenda pia alikuwa anamfikiria zaidi mshindani wake kwenye mbio za kiatu cha ufungaji bora ambaye ni Aziz Ki kuliko kitu kingine chochote kile.

Na hata baada ya mpira kula nguzo Fei alikuwa na reaction ya huenda kila kitu kwake kimeishia pale na hakuna tena uwezekano wa yeye kufunga tena katika ule mchezo na ndicho kilichomtokea kwa kuwa na yeye anacheza kwa presha kubwa ya kinachoendelea mitandaoni.

Azam FC sasa sio kwamba hawataki Fei achukue kiatu cha ufungaji bora HAPANA lakini kwa sasa nyuma ya camera wajaribu kuongea nae kama ilivyo kwa Yanga pia kuongea na Aziz Ki, Fei apewe morali ya kuwa ana uwezo wa kupata nafasi ya kufunga kwenye mechi nyingine baada ya Simba kupita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live