Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki amfunika vibaya Fei Toto

Fei Toto Amfunika Aziz Ki Ligi Kuu Aziz Ki amfunika vibaya Fei Toto

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo mshambuliaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, Stephane Aziz Ki, anayeongoza kwa kufunga mabao, ameweka rekodi nyingine ya kuwa kinara wa kupachika mabao kwa mipira ya adhabu 'fri-kiki', mpaka sasa.

Kwa mujibu wa takwimu ziliyotolewa na Bodi ya Ligi jana, pamoja na za dawati letu la michezo, Aziz Ki, mwenye mabao 15 katika Ligi Kuu, akiwa sambamba na Feisal Salum, amepachika mabao matatu kwa njia ya faulo, na kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi ya aina hiyo kwenye Ligi Kuu, wakati zimebakia raundi tatu tu kumalika.

Raia huyo wa Burkina Faso ambaye pia ni mmoja wa wanaoongoza kwa kutoa pasi za mwisho za mabao, akifanya hivyo mara nane, pamoja na Kipre Junior na Fei Toto, wote wa Azam, amekuwa na rekodi nyingi nzuri msimu huu, ikiwamo kuongoza kwa kupachika mabao akiwa nje ya boksi, ambapo amefanya hivyo mara tano.

Wakati Aziz Ki, akiwa na mabao matatu ya faulo, nyuma yake yupo Edwin Balua wa Simba ambaye ana mabao mawili ya 'fri-kiki', moja akilifunga akiwa na timu yake ya zamani Prisons, akiifunga timu yake ya sasa, na moja akiwa kwenye klabu yake mpya akifunga dhidi ya Namungo. Mwingine mwenye mabao mawili, ni raia wa Togo, anayewindwa kwa sasa na Simba, Marouf Tchakei wa Ihefu.

Wachezaji waliofunga bao moja la faulo ni, Cheikh Sidibe wa Azam FC, Gadiel Michael wa Singida Fountain Gate, Valentino Mashaka wa Gaita Gold, Ibrahim Ajibu wa Coastal Union, Clatous Chama wa Simba, Martin Kigi na Najimu Magulu wote wa JKT Tanzania, Jeremiah Juma wa Prisons, Dissan Galiwango na David Luhende, wote wa Kagera Sugar, na Omari Kindamba wa Mashujaa FC.

Takwimu zinaonyesha straika wa Singida Fountain Gate, Habib Kyombo, anaongoza kwa kupachika mabao ya vichwa mpaka sasa, akiwa ameshatumbukiza magoli manne.

Mchezaji huyo anafuatiwa na wachezaji waliopachika mabao matatu ya kujitwisha, ambao ni Sadio Kanoute wa Simba, Waziri Junior (KMC), Paul Buswita (Namungo), Elvis Rupia wa Ihefu FC, na Semfuko Charles wa Coastal Union.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: