Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki amerudi kwenye kiti chake cha ufalme

Pacome Aziz KI.jpeg Aziz Ki, Pacome na Yao.

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiwango Bora sana kutoka kwa Stephen Aziz msimu huu ukiacha performance na ufundi wake kunakitu kakiongeza Aziz anashuka ana kaba.

Mwalimu Miguel Gamondi anatengeneza mashambulizi kwa kupitia kwake ndiyo maana ana assist na pia anafunga. Takwimu zake za kufunga msimu huu imeongezeka tena magoli ya uwanjani.

Alianza kufunga katika nusu fainali ya Ngao dhidi ya Azam FC kipindi cha pili juzi kafungwa dhidi ya Asas ya Djibouti na juzi katika mchezo wakwanza wa ligi kuu amewafunga KMC.

Aziz Ki aliwasubirisha wananchi mpaka saa 6 usiku wakati anatambulishwa msimu uliopita, baada ya kutua Jangwani alionesha kiwango kizuri lakini hakikutosha kuwafurahisha Wananchi ikilinganishwa na uwezo wake wakati yupo Asec Mimosas.

Msimu uliopita Aziz alikuwa na mechi chache za kuonesha kiwango wakati baadhi ya mechi alionekana kushuka kiwango chake hali iliyosababisha hata mwalimu Nabi kumfanya kama chaguo la pili kwenye kikosi chake.

Ujio wa mwalimu Gamondi, viungo Pacome Zouzoua na Max Nzengeli umemuamsha Master Key amerudi kwenye kiti chake cha ufalme Jangwani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live