Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki amemuacha mbali mno Fei Toto - Manara

Fei X Aziz Fainali Aziz Ki na Fei Toto

Tue, 4 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanachama wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesikitishwa na tabia ya baadhi ya wachambuzi wakilaumu kwamba mashabuiki wa Yanga hawamkutendea haki kiungo wa Azam FC, Feisal Salum 'Fei Toto'.

Manara amefafanua kuwa watu wanaona nyota huyo aliyewahi kukipiga Yanga SC ni kama anaonewa na anastahili kuwa MVP wa msimu huu.

“Kila mtu anaandika lake. Litakuwa shirikisho la mpira la ajabu kuwahi kutokea Tanzania pengine Duniani, Aziz KI asipokuwa MVP kwa msimu huu na tutaonekana ni wenye vituko kwa namba ( takwimu) baada ya hapo tuzungumzie perfomance ya kucheza na Perfomance ya kufunga zote ameongoza Aziz KI.

“Ukikaa kwenye Tv, macho yako ukiangalia perfomance ya Aziz na Fei macho yako yatafurahia zaidi kumuangalia Aziz Ki hata Fei mwenyewe analijua hilo, ni sawa Fei ni mchezaji mzuri lakini Aziz ni kitu kingine.

"Yani anakupa ladha kumuangalia namna anavyo dribble, namna anavyofanya juggling zake uwanjani na kupiga zile pasi zake na namna anavyo desh,namna anavyopiga yale matobo kwa chenga zake na pasi zake za mwisho ni raha kumuangalia.

"Kwa hiyo ukiacha kufunga kwake namba hizo Aziz yupo mbali kwa Fei, magoli 21 na assist 7 sio kitu cha masihara katika mechi 27 alizocheza amehusika na magoli 28 namba yake ni kubwa mno.

"Ni kweli tunapenda kuona Watanzania wanashinda hizo MVP lakini haiwezekani kwa namba za Aziz Ki tutaonekana tunafanya mchezo kama tunaudhihaki mchezo wa mpira wa miguu itaonekana kitu cha hovyo duniani,” alisema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live