Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki amegundua mabosi wa Yanga hawaaminiki - Edo Kumwembe

Aziz Ki Sta Aziz Ki.

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa soka Edo Kumwembe kutoka Wasafi FM amesema kuwa, kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz KI ameona mabosi wake hawaaminiki, wanaweza kumuacha mchezaji yeyote bila kujali walimnunua kwa pesa kubwa na kumtambulisha kwa mbwembwe.

Edo amesema kuwa, hicho ndicho kimemfanya Mburkinabe huyo kuamua kupambana ndani ya kikosi hicho wakati mkataba wake wa miaka miwili ukielekea ukingoni mwishoni mwa msimu huu.

Aziz Ki ameanza na moto mkubwa ikilinganishwa na performance yake ya msimu uliopita aliposajiliwa na miamba hao wa soka nchini akitokea ASEC Mimosas ya Ivory Coast ambapo kwa msimu huu pekee katika mechi 7 amefunga mabao 6 na kutoa assist moja ya bao.

“Msimu huu inaonekana Aziz KI anasaka mkataba. Lakini hapo hapo amegundua kwamba Yanga hawaaminiki, wana roho ngumu, hawaangalii sana namna ulivyokuja kwa mbwembwe, kumbe wanaweza kukubali hasara na kusonga mbele.

“Ungeweza kudhani Yanga ingeachana na Yanick Bangala hasa baada ya kiwango alichoonyesha katika msimu wa kwanza? Ungeweza kudhani Yanga ingeachana na Djuma Shabani baada ya kelele zote zile za uhamisho wake akiwa mmoja kati ya mabeki bora wa kulia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa akiwa na AS Vita?

“Nadhani Aziz amehisi kwamba kumbe yote haya yanawezekana. Labda ndio maana amepania msimu huu,” amesema Edo Kumwembe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: