Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aziz Ki alishasaini Yanga Kitambo - Jemedari Said

Video Archive
Wed, 10 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi mkongwe wa soka Bongo, Jemedari Said ameweka wazi kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki alishasaini kuendelea kuwatumikia Wananchi kitambo na kilichokuwa kinaendelea mitandaoni ni 'kiki' tu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jemedari ameposti picha ya nyota huyo na kushusha maneno haya:

Tarehe 12 Juni Azizi Ki aliwekewa pesa za Kitanzania Tshs 520M kwenye benki moja hapa nchini na maelezo yake yalikuwa ni pesa ya usajili ambayo haikuanisha ni muda gani aidha mwaka mmoja au miaka miwili.

Pesa ambayo mhusika pia aliitoa baadae kwa matumizi yake mwenyewe kwenye siku hiyo hiyo.

Kinachoendelea mtandaoni ni jambo JEMA SANA kwenye Dunia ya mitandao ili kuleta mvuto na kutengeneza wasiwasi kwa wanayanga na baadae viongozi kuibuka “Mashujaa” kwa kushinda vita ya usajili. Lazima kutengeneza kufatiliwa kwenye social media platforms za klabu kwenye Dunia ya leo.

Mchezaji ambaye hajasajiliwa amekuja kufanya nini kiasi apewe na muda kwenye App ya klabu? Welcome Back King Ki, the world is all yours. Hongera viongozi kwa kumbakisha Top Scorer.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live